Matatizo ya maji Afrika yatakwisha lini?

Tatizo la maji limekuwa sugu barani Afrika ambako ndiko kuliko vyanzo
vyote vya majiikiwamo mto Nile, pich hii inaonyesha mahangaiko ya
wananchi wa Goma katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakihangaika
kutafuta maji.

(Picha kwa hisani ya Ruben Lukumbuka).
Read more...
Watuhumiwa wa Kenya watua “The Hague”

Kutoka upande wa nyuma waziri wa zamani wa elimu William Rutto,
waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgey na mtangazaji Joshua Arap Sang
wakiwa mahakamani “The Hague”.
Wakenya watatu wameshutumiwa kwa kula njama za ghasia za baada ya
uchaguzi za mwaka 2007 na 2008 na wamefikishwa mahakamani kwa kujibu
kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi huko ICC.
Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) waziri wa zamani wa elimu Bw.
William Rutto , waziri wa viwanda wa zamani Henry Kosgey na mtangazaji
wa radio Joshua Arap Sang walikuwa mahakamani huko Hague jana alhamisi
kujibu mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Wakenya wengine watatu wamepangwa kwenda mbele ya mahakama hiyo.
Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo amewashutumu watu
wote sita kwa kuandaa ghasia hizo ambazo zimeuwa watu 1,300 na
kusababisha wengine 300,000 kupoteza makazi yao.
Read more...