Posted by Unknown | 0 comments

Watuhumiwa wa Kenya watua “The Hague

Watuhumiwa wa Kenya watua “The Hague”


Kutoka upande wa nyuma waziri wa zamani wa elimu William Rutto, waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgey na mtangazaji Joshua Arap Sang wakiwa mahakamani “The Hague”.
Wakenya watatu wameshutumiwa kwa kula njama za ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007 na 2008 na wamefikishwa mahakamani kwa kujibu kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi huko ICC.
Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) waziri wa zamani wa elimu Bw. William Rutto , waziri wa viwanda wa zamani Henry Kosgey na mtangazaji wa radio Joshua Arap Sang walikuwa mahakamani huko Hague jana alhamisi kujibu mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Wakenya wengine watatu wamepangwa kwenda mbele ya mahakama hiyo.
Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo amewashutumu watu wote sita kwa kuandaa ghasia hizo ambazo zimeuwa watu 1,300 na kusababisha wengine 300,000 kupoteza makazi yao.

0 comments: